HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 January 2013

ETHIOPIA 2 TANZANIA 1





Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo (Januari 11, 2013) kwenye Uwanja wa

Addis Ababa hapa jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi

kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua

sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji

watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki

mmoja wa Ethiopia.

Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili

akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.

Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius

Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum

Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
Addis Ababa

YANGA YAKUNG'UTWA TENA UTURUKI


Young Africans imepoteza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi baada ya kufungwa kwa mabo 2-0 katika mchezo uliofanyika katika mji wa Bereke kwenye viwanja vya Arcuda foootball Antalya.

Young Africans ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kufunga lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Nizar Khalfani, George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga kupata bao katika dakika 15 za kwanza,

Dakika ya 23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.

George Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa uwanja.

Mlinda mlango wa Yanga Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya hatari langoni mwake baada ya washambuliaji wa Emmen kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa Yanga lakini mashuti yao walikuta yakiishia mikononi mwake.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Emmen FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.




Yanga ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.

Emmen FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73 waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi iliyowapita walinzi wa Yanga.

Dakika nne (4) baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka mlinda mlango Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya mshambuliaji wa Emmen FC haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.

Jerson Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga kubadilisha matokeo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Young Africans 0 - 2 Emmen FC.

Mara baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na matokeo hayo, timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.

Makosa yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo itakayofuata alisema 'Brandts' .

Yanga kesho itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na safari ya nchini Tanzania siku ya jumapili mchana ambapo itarajiwa kufika Dar es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya jumatatu alfajiri.

Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika, Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima

Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende

WACHEZAJI WA ZAMANI WAJAZWA BINGO NA NMB


Benki ya NMB imekubali kudhamini bonanza la wachezaji wa timu zilizowahi kushiriki daraja la kwanza linalotarajiwa kuchezwa januari 13 mwaka huu kwenye viwanja vya Sigara, Temeke.

Akizungumza jijini Mratibu wa bonanza hilo Kenedy Mwaisabula alisema tunatoa shukrani za dhati kwa banki ya NMB kwa kutambua mchango wa wachezaji wakongwe katika taifa hili na kukubali kuwapa sapoti.

"Tunaishukuru benki ya NMB kwa kutambua mchango wa wachezaji wa zamani kwa kukubali kudhamini bonanza hili", alisema Mwaisabula.

Timu za zamani ambazo zinashiriki kwenye bonanza hilo ni zile zilizowahi kutamba hapa nchini katika ligi kuu ya Tanzania ( zamani ligi daraja la kwanza) na litaanza saa 2:00 asubuhi, zinatakiwa kukamilisha ytaratibu zote ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya ushiriki.

Timu hizo ni Simba, Yanga, Ushirika, Tukuyu stars, Pamba ya mwanza, Bandari ya Mtwara, Reli ya Morogoro, Pilsner, Coastal union, Kariakoo Lindi.

Pia alisema timu za simba, Yanga na Bandari ndio zimelipa ada za ushiriki hivyo kuomba zilizobaki kulipia mapema na amewataka mashabiki kufika kwa wingi kujionea burudani ya kandanda safi toka kwa wachezaji hao wa zamani.

Bonanza hili ni la pili kufanyika baada ya lile la kwanza lililofanyika Novemba 18 mwaka jana, ambapo Milambo ya Tabora ilifungwa magoli 3-2 na Bandari Mtwara, Reli Morogoro iliifunga Plisner ya Dar 1-0,Simba ilitoka sare na Kariakoo Lindi ya mabao 2-2 na Ushirika Moshi ilicheza na Kombaini baada ya kuwa na timu saba

(LIVE)MAPINDUZI CUP LIVEEE NDANI STAR TV KESHO AZAMA VS TUSKER DIGITAL






Kampuni ya kutengeneza vyakula na vinywaji ya SSB ambayo pia ni wadhamini na wamiliki wa klabu ya Azam FC wameingia kandarasi na kituo cha televisheni cha Star TV kurusha matangazo ya mchezo wa kesho wa fainali ya Mapinduzi Cup

Fainali hiyo ambayo itawakutanisja mapingwa wa Kenya Tusker FC na Mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup Azam FC itachezwa kwenye uwanja wa Amaan usiku wa kesho kuanzia saa mbili na nusu

Katika mchezo wa Kesho, mbali na wachezaji waliopo Ethiopia na timu ya Taifa, pia Azam FC itawakosa wachezaji wake sita muhimu wanee wakiwa na majeruhi na wawili wakitumikia adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya nusu fainali.

Wachezaji watakaokosekana ni Aishi Manuala (Timu ya Taifa) Waziri Salum (majeruhi) Ibrahim Mwaipopo na Jabir Aziz (Kadi Nyekundu) Abdulhalim Humud na Abdi Kassim (Majeruhi) Salum Abubakar na Hamis Mcha (Timu ya Taifa) John Bocco na Kipre Tchetche (Majeruhi)

DR SHEIN ATISAINI UZINDUZI WA "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA"


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitia saini Mpira katika uzinduzi wa Mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",mradi ambao utawapatia vijana wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu ,(20,000) katika vikundi mbali mbali na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka nchini,katika sherhe za kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)

Baadhi ya Watoto wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti unaosisitiza kulindwa haki zao,wakipita kwa
maandamano mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", zilizofanyika jana katika Uwanja wa Amaan Studiuam,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea kitabu kutoka kwa Nasra Sheikh Mohamed,wa Skuli ya Mwembeshauri Mjini Unguja,kitabu chenye Agenda ya Watoto kuhusu usisitizaji kwa Serikali na Jamii kushirikiana katika kuwapatia haki zao za Msingi bila unyanyasaji. katika uzinduzi wa Mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",katika uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Paulo Edwards, katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA" ,katika Uwanja wa Amaan Studium, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)

SIMBA YAANZA MAZOEZI OMAN



Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba wameanza Mazozei  nchini Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Simba iliondoka  jijini juzi kuelekea Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
Katibu  mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amesema wachezaji wote wako imara na wanaendelea vyema na mazoezi.

 Simba imepanga kucheza mechi tatu za kirafiki kabla ya kurejea nchini kuanza mzunguko wa pili wa ligi na kwamba katika mechi ya kwanza wataikabili timu ya Fanja FC ya Oman.

Akizungumzia kuhusu kutolewa katika Kombe la Mapinduzi amesema hatua ya kupigiana penalti ni ya bahati kwa upande wowote.

"Kikosi kilionyesha uwezo mkubwa, lakini bahati haikuwa yetu," .

Aliongeza kuwa wanaipongeza Simba kwa hatua waliyofikia na kuwataka wachezaji wasivunjike moyo na kushindwa kufika fainali.

Aliongeza kuwa  wameshaufunga ukurasa wa michuano hiyo na sasa wanajipanga kuwasafirisha wachezaji waliobaki kwenye michuano hiyo ili wakaungane na wenzao 14 waliotangulia kambini Oman.

Simba ambayo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu itarejea nchini baada ya wiki mbili kwa ajili mzunguko wa pili wa ligi kuu inayotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi katika viwanja tofauti nchini.

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers