HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 February 2014

MALINZI AVUNJA MKATABA NA KIM POULSEN LAKINI!!!!!
Shirikisho la mpira  wa miguu la Tanzania tff limevunja mkataba na aliyekuwa mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen  ,Rais wa tff Jamal Malinzi amesema kuwa wamekubaliana  kuvunja mkataba kwa makubaliano maalum na ni siri  kati ya Shirikisho na kocha lakini amesema serikali inatambua kuhusu hari hiyo.


Licha kubanwa na maswali ya waandishi wa habari rais wa tff bado hakutaka kuweka hadharani ni kiasi gani kimeigharimu Tanzania kulipa pesa za kuvunja kandarasi hiyo ambayo ilibidi imalizike 2015 kwa upande mwingine inaonekana wazi kuwa kocha anayekuja kuifundisha Tanzania anaweza kutokea uholanzi kwani baada ya kubanwa na waandishi wa habari ataje angalau nchi anayotoka kocha anayekuja alitaja nchi ambazo ujerumani ambayo ina kocha mmoja na uholanzi makocha wawili ambao wamebakia katika mchujo unaoendeshwa na chama hicho.


Aidha kwa upande wake Kim alionekana kutoa Tathmini ya  mafanikio aliyoyapata tangu alipoteuliwa  kuifundisha stars  huku akionekana kutetea CV yake lakini akaweka wazi kuwa wachezaji wa kitanzania ni wafupi na wavivu wa kula ndio maana walipocheza na Ivory coast iliwapa sana tabu na matokeo yake wakapoteza mchezo lakini ameipongeza Ivory coast kuwa ni timu nzuri na inastahiri kucheza kombe la Dunia.


Na yeye alipoulizwa kuhusu gharama ya kuvunja kandarasi hiyo majibu yalikuwa ni yale yale aliyotoa Rais Malinzi huku akitilia mkazo kuwa katika ofisi yoyote lazima kuwe na mabadiliko.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers