HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 March 2014

KOMBE LA DUNIA LA WATOTO WALIOTELEKEZWA LATIBA YAPANGWA



 
Makundi ya Michuano ya Kombe ya Dunia kwa Watoto wa Mitaani yamepangwa ambapo   Tanzania (Street Stars) imepangwa kundi la 2 ambalo linaonekana kuwa kundi gumu sana. Mashindano hayo yatafanyika nchini Brazil katika Jiji la Rio de Janeiro kuanzia tarehe 28/03/2014 hadi tarehe 7/03/2014. 
Kundi la Tanzania lina timu za 
1. Tanzania 2. Burundi 3. Argentina 4. Philippines 5. Nicaragua Makundi mengine ni  Kundi la kwanza lina timu za 1. Brazil 2. South Africa 3. Liberia 4. Indonesia 5. Egypt Kundi la tatu lina timu za 1. Kenya 2. Mauritius 3. USA 4. India 5.

 Timu ya Tanzania iliyokuwa ikinolewa na Sylvestre Marsh kabla ya kuugua, itaondoka Tanzania tarehe 27th baada ya Kuagwa na Serikali ikiwa na msafara wa viongozi 3 akiwemo Mwalimu wa timu, na Rais wa TSC Sports Academy Bw. Altaf Hirani, na wachezaji 10 wa umri chini ya miaka 16 pamoja na wachezaji waandamizi 2 walioshiriki mashindano haya mwaka 2010 kule Durban Afrika Kusini.

 Ikumbukwe kuwa Tanzania inashiriki mashindano haya kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushiriki kule afrika kusini na kufanikiwa kufika fainali baada ya kuzifundisha soka  timu za, Brazil,  Phillipines ,  Nicaragua , na baadae kutoka sare na Uingereza moja moja, kabla ya kufungwa na India kwenye fainali goli moja bila, Tanzania ikifungwa kwa mkwaju wa penalt zikiwa bado dakika 5 mpira kumalizika. 

Kwa kumbukumbu hii Tanzania inaelekea Brazil ikiwa na dhamira moja tu kushinda kombe hili na kulileta Nyumbani.
 Mutani Yangwe (Mwanzilishi na Mkurugenzi wa TSC Academy) ambaye yupo nchini Uingereza ataondoka kuelekea Brazil tarehe 26 kwa ajili ya kuipokea timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers