HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 March 2014

KEVIN FRIDAY AMTESA JUMA KASEJA TAIFA

http://4.bp.blogspot.com/--WrzuS-ifQo/Uym6E5azNiI/AAAAAAAA8TY/1JuI4QfAKgk/s1600/_DSC0053.JPG
ISSAH MICHUZI PICTUREKlabu ya soka ya yanga imekwenda suluhu ya kufungana Goli moja kwa moja na Azam fc katika mchezo wa ligi soka Tanzania bara na kuemdelea kushika nafasi ya pili huku Azam wakiwa katika nafasi ya kwanza na alama 44 huku yanga wakifikisha alama 40 Didier Kavumbagu aliipatia Yanga goli kuongoza baada Piga nikupige katika goli la Azam katika dakika kumi na nne ya Mchezo.

Aidha Klabu ya yanga ilizawadiwa mkwaju wa Pernati baada ya mlinzi wa Azam kuunawa mpira katika Eneo la kisandulku cha Penati lakini Penati hiyo iliotambawa baada ya Hamis kiiza Diego kukosa huku mlinda mlango wa azam aishi manura akiicheza penati hiyo lakini baada ya kupigwa penati Mlinzi wa Azam fc Erasto Nyoni alitandikwa kadi Nyekundu kwa kilichooneka kumfokea mwamuzi.

Lakini katika Dakika ya Themanini na Tatu mpira safi ulioanza katikati ya kiwanja na kumkuta Jonh Boko na kumiminia Sure huku Kevin Friday akiuomba mpira kwa ishara ya mikono miwili alikung'uta bakora ambayo hata kama kungekuwa na kaseja wawili wasingeweza kudaka shuti ile na kuisawazishia Azam goli mpaka mwisho mchezo Azam 1Yanga1

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers