HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 March 2014

MASHABIKI WA SOKA TANZANIA WANAPOWASHINDA NGUVU VIONGOZI WA SOKA 
Leo natazama jinsi mashabiki wanavyoweza kuwazidi nguvu viongozi wa soka la Tanzania naama bila shaka unaanza kusoma kwa hamu sasa nakujiuliza ni nguvu ya aina gani hiyo?

Ninaposema mashabiki wanawazidi viongozi kimaamuzi ni pale unapotazama ufanyaji kazi wao, Mtu  pekee aliyewahi kuja Tanzania na kufundisha soka marcio maximo , aliyemwka mtu anayedaiwa kuwa mlinda mlango nambari Juma Kaseja kwa utovu wa nidhamu licha ya kupigiwa makelele na mashabiki wa soka Marcio hakubadirisha msimamo kiasi cha kuchukiwa na baadhi ya mashabiki wa timu aliyokuwa akichezea .

Leo hii wapo baadhi ya viongozi wa kitanzania ambao wameshindwa kusimama  kidete kufumba macho na kutupilia mbali kile ambacho mashabiki  wa soaka wanataka , katika soka la Tanzania mashabiki wananguvu kubwa sana na ukiwafwatisha wanaweza kukupoteza kabisa kwani hata kama wazo walitoa wao ukifungwa watakubadilikia tu watasahau kama wao ndio walio kushauri.

Yapo mambo ambayo yameshafanywa katika shirikisho la soka la Tanzania kama kuanzisha mfumo wa Muda mfupi kama anavyoita Rais wa tff Jamali malinzi sina maana ya kutofautiana kimaamuzi bali ninantofautiana nae kimawazo kwani unaweza kuamua bila kufikiria wakati mwingine.

Sioni haja yakuwa na haja mchakato wa muida mfupi kwani kama timu ya taifa ya Tanzania ipo young taifa stars ipo kuna haja gani ya  kutafuta wachezaji kutoka kila eneo la Tanzania hii leo  kwa kutumia maimilioni ya shiringi kwani wale vijana wa miaka yote ya Copa coca cola wamekwenda wapi  nia ya malinzi imekuwa kutaka kuleta timu ya taifa yenye sura ya muungano binafsi yangu nina jaribu kutazama ni lini timu ya taifa imeshindwa kuwa na sura ya muungano au ni hoja za kisiasa za kutaka watu wa Zanzibar wamuone kuwa wamepata mtu anayewajari sana .

Pengine malinzi hajui  pengine hajawahi kukaa na wazanzibar mimi ninamsaidia leo hii Wazanzibar wanachotaka sio hicho wnataka Uanachama Fifa sio kingine hawana mpango  wa kutaka  timu ya taifa ya pamoja kila mwaka wamekuwa wakiona wachezaji wao wakicheza katika timu ya taifa ya Tanzania lakini sio wengi kiasi hicho .

Hapa ndipo ninaposema kuwa anazidiwa na maamuzi na washabaiki viongozi wanakwenda kutokana na nguvu ya mashabiki .sio nguvu zao za   Binafsi viongozi wengi wa soka la Tanzania wanatazama upepo wa mashabiki wanataka nini mechi zinapochezwa kiwanjani mabo mengi  hufanywa kutoka  na nguvu ya mashabiki majukwaani je? Unafikiri tutafika .

Mwaka elfu mbili na mbili rais wa Brazil Da Silva aliwahi kumwambia Luis felipe Scolari  kama hatomjumuisha Romario De souza na kutokuchukua ubingwa basi  asirudi Brazil lakini Big Phil alishikiria msimamo wake na kumwacha De souza na wakachukua ubingwa.

Lakini kwa Tanzania viongozi  wengi wanashindwa na nguvu na mashabiki na kufanya  kazi kwa upepo wa  mashabiki ukikaa jukwaani na kusikiliza mashabiki wao tayari ni makocha kabla ya kuwa makocha .

    Je kuna haja ya kwenda kushiriki michuano ya mataifa ya afrika tu kwanini tusiwe na lengo la kujenga mifumo ya soka kwanza shida iliyopo kila mmoja katika uongozi anataka kufanya jambo nili akumbukwe kuwa alitufikisha mahala fulani wakati mwingine hizo huwa sifa za  ambazo haziwasaidii watanzania .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers