HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 March 2014

MAZINGIRA YA SHULE ZA TZ HAYAMSHAWISHI MZAZI KUMWACHA MTOTO AJIKITE MICHEZONI(SIKIZA SAUTI)






SIKIZA SAUTI HAPA







Leo hii nimepita katika shule ambayo nilisoma kuanzia Darasa la kwanza  mpaka la Saba  shule ya msingi Mtakuja shule  ambayo imenikuza, nilikwenda kutembelea  kutazama sera ya michezo inavyotekelezwa  shuleni hapo  kwa hakika ukifika tu shuleni hapakupi  hamu ya kufikiri kuwa kuna harakati zozote za michezo katika shule hii na hapo ndipo unapoona kuwa ndoto za Tanzania kushiriki michuano  mikubwa ya  kimataifa hasa ya vijana .

Ni kweli kabisa unavyoona hapo pichani sidhani kama kuna mzazi ambaye anataka kumpeleka mwanafunzi katika shule kama hiii walio wengi wanaopeleka watoto wao hapa uwezo wao ni wa chini sana katika kipato chao cha kifedha na ni wanafunzi wachache sana ambao hufanikiwa kusonga mbele zaidi hata kielimu.

Ni jambo la kawaida sana kusikia katika vyombo vya habari kuwa michezo inapigiwa upatu kuwa imerejeshwa lakini ukitazama sio kwa asilimia mia moja kwa sababu kama kipindi cha michezo hakuna sio rahisi kwa wanafunzi kama hawa kuweza kuelewa nini kinachoendelea katika ulimwengu wa michezo  kwa hakika wanafunzi wengi wanawajua wachezaji wa kimataifa  nyakati nyingine  unaweza kushangaa wanayajua vipi.

Lakini kama mwanafunzi anaweza kunasa mchezo mzima wa mpira wa miguu ambao unaooneshwa katika televisheni na kukuelezea kila kitu ni rahisi sana kama angepata mafunzo ya kipindi cha michezo kikafundishwa kuhusu kwa ujumla na mchezo aupendao kwa dakika japo thelathini kila mwisho wa wiki lakini bado jambo hili hakuna katika hari ilivyosasa ni vigumu sana kuinua michezo Tanzania

Nimefanya mazungumzo na Na mwalimu wa michezo katika shule ya msingi Mtakuja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Chirwa ambaye yeye binafsi na mwenyeji wa Ruvuma

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers