HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 March 2014

MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA
MBEYA City imerudi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers jioni hii Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mbeya City sasa imetimiza pointi 39, moja zaidi ya Yanga SC inayoshuka kwa nafasi moja hadi ya tatu, baada ya kucheza mechi 21. Yanga imecheza mechi 17.
Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Saad Kipanga mawili dakika za nane na 24 na lingine Deus Kaseke dakika ya 34, wakati Yohana Maurice alijifunga dakika ya pili kuipatia Rhino bao la kuongoza.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, bao pekee la Ayoub Kitala dakika ya 63 limeipa ushindi wa 1-0 Ruvu Shooting dhidi ya JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Ruvu Shooting inatimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 21 na inapanda hadi nafasi ya saba, wakati Oljoro inabaki nafasi ya 13 na Rhino inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 14.
Wenyeji Coastal Union wameshindwa kuutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Mkwakwani, Tanga baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Ashanti United jioni hii.
Matokeo hayo yanaiongezea Ashanti pointi moja na kutimiza 18 katika mechi 21 hivyo kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11, ikiishusha JKT Mgambo nafasi ya 12.
SOURCE BIN ZUBERY 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers