HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

21 March 2014

MECHI YA KIHISTORIA MAN U DHIDI YA BAYERN MUNICH ROBO FAINALI UEFA

 

Ratiba ya klabu bingwa barani ulaya imepangwa mchana wa leo huku ikikutanisha mechi za kihistoria na mambo mengi ya kukumbuka.
Mechi ya kwanza itakutanisha maasimu wakubwa katika soka ya Uispania kati ya , Barcelona vs Atletico Madrid, mechi ambayo itakuwa na kandanda maridhwa .

Mechi ya pili itakunisha nusu fainali ya msimu uliopita kati ya  Real Madrid vs Borussia Dortmund ikiwa kama mchezo wa kisasi kwa timu zote mbili , huku  Real Madrid wakitolewa katika michuano hiyo mwaka jana katika hatua ya nusu fainali Dhidi ya Dortmund.

Mechi ya Tatu itakutanisha kati ya  PSG Dhidi ya  Chelsea, huku timu zote zikimilikiwa na matajiri moja ikitoka katika jiji la  London, Na  wengine wakitoka katika jiji la  Parisian , huku timu zote zikiwa na mastaa wa dunia .

Mechi ya Nne ni ile itakayo wakutanisha Mabingwa wa Uingereza Machester United, na Miamba ya Ujerumani  Bayern  Munich, Katika mechi inayokumbusha matukio mengi ya fainali ya mwaka 1999, ambapo mabingwa wa kufunga dakika za mwisho walipo sawazisha na kupata ushindi wa magoli mawili katika dakika za mwisho.
Ratiba kamili hii hapa 
  • Barcelona vs Atletico Madrid
  • Real Madrid vs Borussia Dortmund
  • Paris St. Germain vs Chelsea
  • Manchester United vs Bayern Munich

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers