HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 March 2014

UGAIDI NA USALITI WA SOKA TANZANIA!!!!

 





Katika hari isiyo yakawaida unapokuwa katika uwanja wa taifa Goli linapofungwa au kukoswa utaskia kelele nyingi za furaha au kwa mashabiki ambao ni zaidi ya Elfu arobaini katika uwanja wa taifa lakini je hawa wanaoshangilia wanaelewa wanachoshangilia kwani mara kadhaa hutokea kufungwa magoli ya ambayo hata kipofu hawezi kukosa na mtu anayekosa ni mtu ambaye anaaminika sana katika timu au kufanya Madhambi ambao pengine huwezi kuamini .

Ugaidi wa soka la Tanzania upo katika maeneo mengine na yapo mambo yanayofanyika Ndani ya kiwanja na nje ya kiwanja lakini kikubwa ambacho watu wanatakiwa kuelewa ni kuwa yanayofwanya nje ya uwanja yanaathari kubwa zaidi ambayo Mashabiki wengi wanaokaa majukwaani hawajui maskini ya Mungu nini kinaendelea  ndani ya kiwanja na laiti wangejua sidhani kama wangekuwa wanakwenda kiwanjani kutazama huo mpira wenyewe.

 jambo la kwanza kwanini simba na yanga zimekuwa zikigombana sana zenyewe kwa zenyewe kuhusu wachezaji katika hasa wakati wa usajiri na kujaa fitna nyingi sana ,na mwisho wa siku Eidha kuishia kutocheza kabisa mpira wenyewe lakini yafuatayo yanaweza kusababisha hari hiyo, Upangaji wa matokeo uliokithiri,uchawi,mapenzi ya timu unayoshabikia  haya ni mambo yanaisibu soka Tanzania.

Kwa ulaya sio rahisi na ukigundulika Ni hatari sana unawezafungiwa maisha yako yote kujihusisha na soka kabisa kwa Tanzania Mchezaji anaweza kuwa Mwanachama wa simba na akawa anacheza yanga na kwa hari ya kitanzania mambo haya ni magumu sana wewe msomaji wa kawaida kuyaamini lakini nina kuhakikishia ya kuwa Mechi nyingi za ligi kuu ya Tanzania kwa asilimia 70 Matokeo yanaweza julikana kabla hata ya mechi kuchezwa. na hii ni kwa miaka mingi imetokea  na tatizo hili alijaanza leo ni kwa muda mrefu sasa mambo haya yanafanyika japokuwa kunaweza kusiwe na ushahidi wa kutosha wa hari hii.

Ni kwa hari hii mamilioni ya watanzania huzungumza soka kwa undani pasipo kujua nini kinaendelea hasa mashabiki wa wanaosoma magazeti na kukaa vijiweni na wengine wakithubutu kuwafananisha wachezaji wao na wachezaji nguli wa kimataifa labda kabla sijaenda mbali nikupe nukuu hii ya Mchezaji mmoja aliyetoka klabu moja kubwa na kwenda klabu nyingine kubwa.

Mfano Mchezaji anaweza sema hivi “Mimi mpira ni kazi yangu kama Simba wakihitaji msaada kwangu nitawasaidia na kwenda Yanga kucheza mpira” Je kauli hii unaeielewa waje msomaji wangu? .

 Soka ya Tanzania ina usaliti wa hari ya juu mnawezaje kufanya mazoezi kiwanjani kwa uaminifu na kujipinda lakini kwenye mechi anapitwa kirahisi kabisa pasi na hata kujishuhurisha hata Chembe  je haya ninayokueleza huoni kama ni usaliti ulio kithiri mashabiki hawajui kamati za ufundi na wanachama na viongozi na kama za utendaji zina kazi gani asilimia kubwa ya wachezaji wote wanaocheza katika timu za ligi kuu Bara ni Simba na yanga kiushabiki na wengine wanachama wa klabu hizo .

Sasa huoni kama kuna usaliti hapo  unaweza kuona kama natania katika kueleza mambo hayo kwa muda mrefu Bingwa wa Ligi ya Tanzania sio halisi, na kuna fitna za hari ya juu lakini maskini ya Mungu mashabiki wa hari ya juu huwa hawaelewi nini kinaendelea ndani na nje ya kiwanja.  

Usaliti upo kwa wachezaji na Viongozi na maskini ya Mungu makocha wa Kigeni na huwa hawajui hujikuta wakistaajabu matokeo ya uwanja bila kujua kinachoendelea hii ina maana  kuwa soka Huchezwa kabla ya kuchezwa.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers