HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 March 2014

TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA

 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.

Shughuli inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja wa mpira wa miguu na majukwaa yake.

TFF imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa yake.

Pia Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial ground) mjini Moshi.

TFF inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo ya kujenga vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, waongeze jitihada za kufanya hivyo, TFF itawaunga mkono.

TFF inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu.

TFF inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu haitasita kufanya hivyo.

Wakati huo huo, TFF inalishukuru Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa kukubali kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa Kaitaba, na pia kusaidia uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers