HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 April 2014

Martinus Ignatius "Mart" Nooij ATAIWEZA SOKA YA TANZANIA ?

 
Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.

Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nooij aliwahi kuwa mkufunzi wa Maendeleo wa chama cha soka cha kifalme cha uholanzi  na aliwahi kufanya kazi katika klabu ya EVC 1913 huko marekani na Kazakhstan.Aliwahi kuwa kocha wa Timu ya taifa Burkina Faso chini ya miaka U-20 mwaka  2003 Katika michuano ya kimataifa ya dunia. Mwaka  2004 aliwahi kuwa kocha msaidizi wa muda wa klabu ya nchi mwake ya FC Volendam.
Mwaka 2007 alichaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Msumbiji na alifanikiwa kuipeleka timu hiyo katika michuano ya kimataifa ya mataifa ya afrika mwaka  2010  baada ya miaka 12 . Msumbiji ilimaliza ya mwisho katika kundi lake ikitoa suluhu moja na na kufungwa katika kundi lake Baada ya kushindwa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mataifa mwaka   2012 katika mataifa ya afrika , Nooij alijiuzulu kama Meneja mwaka mwaka  2011. Na nafasi yake kuchukuliwa  na Kocha wa ujerumani  Gert Engels.
Na Tarehe  19 April 2012, alichaguliwa kuwa kocha wa klabu ya soka ya Santos Lakini akafukuzwa kazi   Tarehe 18 December 2012

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers