HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 April 2014

POCHI YAKWAMISHA SAFARI YA TANZANIA TUNISIA -WAVU
Timu ya  za mpira wa wavu za Tanzania Zimeshindwa kuthibitisha ushiriki wao katika michuano ya afrika inayotarajiwa kuanza kesho Nchini Tunisia kutokana na ukata mkubwa wa kifedha unaoukabiri Chama hicho .

Mwenyekiti wa TAVA  Agustino Agapa amesema hakuna fedha kwani walitakiwa kusafirisha timu kwa gharama zao binafsi na kushindwa kumudu safari hiyo.
“Anasema kuwa walitakiwa kuthibitisha ushiriki wao katika michuano ya afrika mashariki ,na kuongeza kuwa wameshindwa kwa sababu hawana pesa za kuwasafairisha na amesema watajipanga kwa safari ya mwakani.

Aidha klabu mbalimbali zinajipanga kwa ajiri ya mashindano ya muungano yatakayofanyika Zanzibar kuanzia wiki ijayo.
            Ni timu saba za wanaume  na wanawake ambazo zimethibitisha kushiriki kwenye mashindano  ambayo yanalengo la kuunga mkono na kuendeleza mahusiano ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers