HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 April 2014

MAN CITY YASHIKWA PABAYA ,PALACE YAIPA ARSENAL AHUENI

Fernandinho


Manchester City imepoteza alama mbili katika kuwania ubingwa ligi kuu soka uingereza baada ya kutoka suluhu ya magoli mawili kwa mawili dhidi ya Sunderland.
almanusura city ipoteza mchezo huo ambapo walipata bao la kuongoza lilofungwa na  Fernandinho, lakini mchezaji wa Sunderland  Connor Wickham alifunga magoli mawili ndani ya dakika kumi na kuipa uongozi timu yake ya Sunderland kabla Samir Nasri kusawazisha katika dakika za majeruhi. sasa city wapo alama sita nyuma ya vinara wa ligi hiyo Liverpool yenye sabini na saba wakiwa michezo 34  na alama nne nyuma ya Chelsea yenye alama 71 baada ya michezo 34
huku  city ikiwa na mechi mmoja mkononi .

Jason Puncheon 
 
Everton imeirejeshea nguvu Arsenal katika kuwania nafasi ya nne ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kukubali kipigo cha magoli matatu kwa mawili dhidi ya Crystal Palace na kuvunjwa kwa Takwimu yao ya kutofungwa kwa mechi saba mfululizo .
Jason Puncheon's na cott Dann's  waliipatia  Palace uhai baada ya kufunga kila mmoja na baadae  Steven Naismith's kusawazisha .
Cameron Jerome aliongeza bao la tatu kwa tai hao wekundu na njano lakini   Kevin Mirallas' aliifungia timu yake goli la kufutia machozi kwa shuti kali katika mchezo uliokuwa safi na wa kuvutia muda wote .
Hii ina maana  Toffees wanabakia katika nafasi ya Tano ,wakiwa alama moja nyuma ya arsenal  ,huku timu zote zikiwa zimesariwa na mechi nne  .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers