HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 August 2014

JOGOO AKATWA MAINI ETIHAD ,BALOTELI ASHUHUDIA JUKWAANI .

 Sergio Aguero
 
Manchester City imeendeleza Rekodi  ya Asilimia mia moja ya kuanza vizuri katika Ligi kuu ya Uingereza katika harakati zao za Kutetea Ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza kwa Kuifunga  Liverpool bao tatu kwa moja .

City ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango Mara Baada ya  Stevan Jovetic kufunga akitumia mwanya wa walinzi wa   Liverpool kuokoa mpira vibaya kutoka kwa mchezaji aliyecheza kwa  mara ya Kwanza Alberto Moreno na  kuumpa nafasi  ya kumfunga  Simon Mignolet. 

Jovetic alifunga bao la pili  ,akipokea pasi iliyorejeshwa Nyuma na   Samir Nasri's , na baadaye Sergio Aguero akitokea kwenye Benchi alifunga bao la Tatu akipokea pasi kutoka kwa Jesus Navas's. 

Majogoo hao wa Anfield walikuwa wageni wa Man city , Huku mchezaji waliye mnunua kwa Dau la Pauni milioni  £16m  Mario Balotelli akiutazama mpira huo katika majukwaa ya watazamaji , Liverpool ilirejesha goli moja baada ya  Pablo Zabaleta's kujifunga dakika za mwisho wa Mchezo . 
Man city 3-1Liverpool 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers