![]()  | 
| Gwiji la soka la Real Madrid Ruben Dela Red akifunga penati na kuifungia Timu hiyo bao la Tatu katika mchezo wa Bonanza lilokutanisha kati ya wachezaji wa Real Madrid na Tanzania 11 | 
Ruben Dela red ameifanyia Maangamizi 
Tanzania 11 iliyokuwa ikifundishwa na Charlse Boniface Mkwasa pamoja na 
Jamhuri kiwelo katika mchezo kirafiki uliokutanisha wachezaji wa zamani 
wa Real madrid na Tanzania 11 .
Real ndio waliokuwa wa kwanza kupata 
Goli katika Dakika ya Kumi ya Mchezo pale Christian Karembeu 
alipoanzisha mashambulizi hadi kwa Luis Figo na baadae kumkuta Ruben 
Dela Red na kumchambua Mlinda Mlango Mohamed Mwameja .
lakini katika Dakika ya 45 ya kipindi 
cha kwanza Tanzania 11 ilisawazisha goli baada ya Real Madrid kujifunga 
katika harakati za kuokoa Robrto Rogers alijifunga mwenyewe baada ya 
kona kuchongwa na Kalima ngonga Ongara mpaka nusu ya kwanza ya mchezo 
Tanzania eleve moja Real madrid moja.
Kipindi cha pili Ruben Dela Red alifunga
 bao la pili  katika dakika ya Themanini ya mchezo na baadae kumaliza 
kwa kufunga bao la tatu kwa njia ya Penati .
Moja kati ya wachezaji waliokuwepo 
katika timu ya Tanzania 11 ni Mohamed mwameja,keneth mkapa ,Boniface 
pawasa,Nasoro Mwinyi Bwanga,peter Manyika,Lunyamila,Dua said,Nsajigwa 
Shadrack,Athuman Abdallah China ,mwanamtwa kiwelo, 
wakati kwa real madrid wachezaji 
wanaojulikana zaidi kwa upande wao alikuwepo fabio canavaro,Christian 
Karembeu ,Luis Figo,Fernando Sanche. 

No comments:
Post a Comment