HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

22 August 2014

LUIS FIGO"ZANZBAR NI PAZURI NITAKWENDA NA FAMILIA YANGU SIKU MOJA. (RADIO PRESS)


BOFYA

Mchezaji wa Zamani wa Sporting Lisbon ,Barcelona ,Real Madrid na Intermillan   na  Mchezaji Bora wa zamani wa Dunia Luís Filipe Madeira Caeiro Figo(Mwaka 2000 ulaya 2001 Dunia ) amesema ipo siku moja atakwenda katika visiwa vya Zanzibar yeye na familia yake kwani ni sehemu Nzuri ya Kutarii.
 
Figo alisema hayo alipoulizwa Swali na mwandishi wa wa Blog ya Dunia ya Michezo kuwa anafahamu kitu gani kuhusu Zanzibar? katika mkutano na Waandishi wa Habari ikiwa ni kabla ya Mchezo kati ya mastaa wa Real Madrid na Tanzania Allstars .

Luis figo ni moja kati ya Mastaa waliotua Nchini kucheza na Kikosi cha Tanzania allstars ambacho kitacheza kesho mechi ya kirafiki katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo anatarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete kuwa Mgeni Rasmi katika Mechi hiyo.

Aidha wachezaji wengine wanaotarajiwa kuwasili leo hii ni kundi la kina Michael Owen pamoja na Macmanam na wachezaji wengine nyota wa Timu hiyo Aidha kwa upande wa kocha msaidizi wa Timu ya soka ya Tanzania Allstars 
Jamhuri kiwelu alberto Pereira amesema anakubali kuwa wachezaji hao wana uwezo mkubwa kisoka lakini watapambana na kiwanjani ili kuwaonyesha kuwa hata wao wanaujua mpira na sivyo kama wanavyodhani na hii itakuwa ni nafasi hata kwa vijana wadogo kujua wakati wao wakicheza walikuwa wakifanyanini kiwanjani.

Mchezo huo utachezwa kesho majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Kwa upande wa Timu ya Tanzania All stars baadhii ya Wachezaji watakao kuwa kikosini ni pamoja na Mohamed Mwameja Jonh mwansasu, yusufu macho na wengine wengi waliowahi kuwika na Real Madrid  .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers