HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 May 2009

POLE didier drogba

Kwa hisani ya BBC Drogba alimwandama Refa kwa matusi Mnamo wiki ijayo mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba atakumbana na adhabu dhidi ya ghadhabu zake baada ya timu yake kupoteza nafasi ya kuingia fainali za kilabu bingwa barani Ulaya. Drogba ameomba msamaha kwa kumrukia Refa Tom Henning Ovrebo kutoka Norway kwa maneno makali. "Nilipandwa na mori na kujikuta ninatamka maneno yasiyostahili. Ninaomba msamaha," alisema Drogba. Essien alifunga bao la Chelsea "Ninakiri kwamba matamshi yangu hayakufaa na hayakutoa mfano mzuri kwa wale waliokuwa wakitizama televisheni, hasa watoto." Chelsea walibaki wakiumwa roho, vichwa na miguu baada ya kupokonywa ushindi wao na Barcelona huku ikiwa imesalia dakika moja na nusu hivi mechi kumalizika. Shirikisho la kandanda barani Ulaya, UEFA, limesema kwamba litatoa uamuzi wake kuhusu tabia ya Drogba wiki ijayo. UEFA ilesema ilikuwa imepokea ripoti ya matukio hayo kutoka kwa Refa na pia wasimamizi wengine wa mechi hiyo. Chelsea walikuwa wakiongoza kwa bao moja lakini hatari ikawa inawanyemelea endapo Barcelona wangefunga bao moja tu na kuongezwa lingine la ugenini. Baada ya dakika 90 ilionekana kama kwamba Chelsea na lao moja walikuwa wanawadia kilele cha kuelekea Roma kukutana na Manchester United kwenye fainali. Lakini penyezapenyeza yao ilibanwa kwa ghafla wakati Andres Iniesta wa Barcelona aliwachilia mkwaju hadi wavuni na kutoboa donda kubwa kwenye nyoyo za wachezaji na mashabiki wa Chelsea. Wachezaji wa Chelsea walimvamia Refa huku wakimshutumu kwa uonevu baada ya kukataa, mara nne, nafasi za penalti dhidi ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers