4 June 2009
RAIS KIKWETE AZINDUA MV MAGOGONI
Pichani ni Mv Magogoni ikitia nanga katika kivuko cha feri ambapo kivuko hicho kimezinduliwa leo na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh jakaya mrisho kikwete
vilele kivuko hicho kimeigharimu serikali shs bil nane na kinauwezo wa kuchukua abiaria mia nane na zaidi ya ishirini
Rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania akushuka kwenye ngani akitoka juu alipokuwa akikagua shuhguri nzima za uendeshaji kivuko hicho
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Jakaya mrisho Kikwete amefungua rasmi kivuko cha Mv magogoni ambacho kitawasaidia wananchi wa kigamboni katika maswala ya usafiri kwani imekuwa kero kutokana na vivuko vilivyopo sasa Mv alina kufanya kazi katika kiwango ambacho hakikidhi matakwa ya wakazi wa kigamboni rais amesema kuwa serikali inafanya kazi kubwa katika kuboresha usafiri wa majini na kuwahaidi wananchi kuwa muda sio mrefu serikali itaanza mchakato wa kujenga daraja ambalo litakuwa la kisasa na kurahisha usafiri kwa wananchi wanaoishi kigamboni pindi wanapotaka kuja Mjini.
Nakata
Rais wa Jamhuri ya muungano akikata rasmi utepe kuashiria kutumika rasmi kwa kivuko hicho
Vilevile mh Kikwete amesema kuwa ule uvumi wa kuwa kigamboni imeuzwa kwa watu maarufu nchini Marekani sio kweli kwani wapo watu ambao hupenda kutunga uongo ambao unawapa faida wanazo zijua wao kwani hamna kitu kama hicho na hakita tokea kwani tuuze kigamboni iliiweje na kwa nini na kwa sababu gani unajua kunawatu ambao hawapendi maendeleo kabisa kwani kwanini tuuze vilevile anakwambia watu wote mtahamishwa sasa mbaya zaidi awaambii mtakapokwenda hamuoni kama ni uongo lakini tatizo kubwa ninyi mnaahamini uongo kuliko ukweli .
Jamani Meli hufunguliwa kwa kuvunja Champain ambayo huvunjwa kwa kupigwa kwenye chuma
Rais wa jamhuri ya muungano akiwa ameshika chupa ya Champain kulia kwa rais ni waziri wa Miundo Mbinu Shukuru Kawambwa
Tupo katika mchakato wa kutengeneza barabara nyingi ambazo zitapunguza adha ya usafiri na msongamano wa magari kwani sasa magari ni mengi lakini sio watu wote ambao wanasafari kuja Mjini lakini kwa sababu njia inapita huko basi lazima wapite.
Rais jakaya kikwete akifungua akitambaa kuonyesha kibao kilicho andika kivuko hiki kimezinduliwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh Jakaya kikwete.
Rais kikwete alipokuwa akihutubia wakazi kigamboni baada ya kuzindua kivuko cha Mv Magogoni
Rais akisalimiana na Baadhi ya viongozi wa wizara ya Miundo Mbinu
Kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wilam lukuvi na Rais kikwete na waziri kawambwa wakiwa kwenye kivuko kuelekea Kigamboni
Ukiangalia kwa mbali utamwona sofia simba akitabasabu bila shaka anafurahia kazi ya bosi wake
Rais kikwete akimpa mkono bi sofia simba alipowasiri kigamboni hii leo wakati wa uzinduzi wa Mv Magogoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment