8 June 2009
Rais Omar Bongo wa Gabon Bado uhai
Imeandikwa na Mwandishi wa BBC
Gabon imekuwa katika uhusiano mzuri wa kiuchumi na Ufaransa
Serikali ya Gabon imekanusha vikali taarifa zilizoendezwa na vyombo vya habari vya Ufaransa kwamba Rais wa nchi hiyo Omar Bongo amefariki dunia.
Waziri Mkuu wa Gabon Jean Eyeghe Ndong amesema Bwana Bongo mwenye umri wa miaka 73 ambaye iliarifiwa ana maradhi ya saratani, "yu hai na mwenye afya".
Serikali ya Hispania ambako kiongozi huyo mwenye muda mrefu madarakani barani Afrika anatibiwa katika kliniki moja, pia imesisitiza kiongozi huyo yu hai.
Bwana Bongo ameiongoza Gabon tangu mwaka 1967, lakini mwezi wa Mei akasitisha kazi zake. Anakabiliwa na uchunguzi wa Ufaransa kuhusiana na tuhuma za madai ya rushwa.
Mwandishi wa BBC mjini Libreville Linel Kwatsi amesema mji huo inaonekana upo kimya kama ilivyo kawaida, hata hivyo baadhi ya watu wameanza kukusanya chakula kwa wingi nyumbani, iwapo maduka yatafungwa kama kifo cha rais kitathibitishwa.
Serikali ya Gabon yenye utajiri wa mafuta imewataka watu kuwa watulivu.
Shirika la habari la Ufaransa-AFP lilitangaza kifo cha kiongozi huyo wa Gabon baada ya kunukuu rubaa za serikali na pia tovuti ya gazeti moja la Ufaransa la magazine Le Point, zikikariri taarifa kutoka kwa walio katika msafara wa Bwana Bongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment