9 June 2009
Rais wa gabon afariki mtoto ali bongo athibitsha
Imeandikwa na Mwandishi wa BBC
Gabon imekuwa katika uhusiano mzuri wa kiuchumi na Ufaransa
Rais wa Gabon Omar Bongo, kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.
Kifo chake kimethibitishwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Jean Eyeghe Ndong katika taarifa ya maandishi.
Kulikuwa na taarifa ya kukanganya mapema siku ya Jumatatu iwapo Bwana Bongo aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani, amekufa katika kliniki moja mjini Barcelona nchini Hispania.
Katika taarifa yake Bwana Ndong amesema Bwana Bongo amekufa kutokana na maradhi ya moyo muda mfupi kabla ya saa sita na nusu mchana siku ya Jumatatu.
Katika mji mkuu Libreville, mwandishi wa BBC Linel Kwatsi amesema watu tayari walikuwa wananunua chakula kwa wingi na kuhifadhi ndani baada ya kuwepo uvumi wa kifo cha Rais Bongo mapema asubuhi ya Jumatatu. Walikuwa na wasiwasi huenda maduka yangefungwa iwapo kifo hicho kingethibitishwa.
Bwana Bongo aliiongoza Gabon tangu mwaka 1967, lakini alishindwa kuendelea na kazi mwezi wa Mei. Alikuwa akikabiliwa na uchunguzi wa serikali ya Ufaransa kutokana na tuhuma za rushwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment