MOTO mkubwa umezuka jana adhuhuri na kuteketeza kabisa Klabu maarufu ya usiku nchini ya Maisha iliyopo Oysterbay wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Moto huo ambao chanzo chake kilielezwa kuwa ni hitilafu ya umeme iliyoanzia katika kiyoyozi (AC) ulilipuka na kusambaratisha kabisa jengo la Klabu hiyo na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Jengo hilo la gorofa moja linalomilikiwa na Watanzania wenye asili ya kiasia, lilianza kushika moto majira ya adhuhuri jana, kuteketeza kabisa mali zote zilizokuwamo ndani yake.Klabu hiyo kongwe na inayosifika kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara za usiku, ipo mkabala na Hoteli ya Karibu, ambapo sasa panajulikana maarufu kwa jina la Morogoro Store.Mwananchi ilifika hapo majira ya saa 8:20 mchana na kushuhudia umati mkubwa wa watu waliokuwa wamefika kushuhudia tukio hilo, huku vikosi cha zima moto cha kampuni ya Knight Support ambacho kiliwahi kufika kikiendelea na uokoaji.Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Meneja wa Klabu hiyo Tongai Muza, alisema moto huo ulianzia katika AC iliyokuwapo sehemu ya baa katika jengo hilo na baadaye kusambaa katika sehemu mbalimbali za jengo.“Moto ulianzia katika AC iliyokuwapo sehemu ya baa ambapo kwanza ilianza kutoka moshi, tukawapigia simu watu wa zimamoto lakini walikuwa hawapokei, baadae ikaanza kutoa moto,” alisema Muza na kuongeza,"alisema. Imeandikwa na Salim Said.
No comments:
Post a Comment