HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

22 July 2010

VODACOM FOUNDATION KUNENEPESHA GALA NIGHT

Meneja wa Mfuko wa Vodacom fondition, Yessaya Mwakifulefule 8kushoto na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali wakizungumza na waandishi wa habari KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali imejitokeza kudhamini maonesho ya mavazi ya hisani yanayolenga kuboresha hali ya mazingira ya Hospital ya wenye matatizo ya akili ZANZIBAR. Maonesho hayo yanayofahamika kama 'Fashion 4 Health Black and Gold Gala' yanafanyika mara ya tatu mfururizo yanaandaliwa na Exprlore ZANZIBAR yatafanyika tarehe 30 Julai mwaka huu katika Hotel ya Serena Inn Mjini humo. "Kwa kuthamini umhimu wa jamii ambayo tunafanya nayo kazi na kwa Heshma ya Maryam Olsen wa Explore Zanzibar tumeshawishika kudhamini onesho hili kuchangia majengo ya Hospitali hiyo," alisema Mwakifulefule. Naye mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mstafa Hassanali alisema katika maonesho hayo atazindua mtindo wake mpya wa mavazi unaofahamika kama 'KARAFUU Collections', akiambatana na wanamitindo wengine 10 kutoka Tanzania bara wakisindikizwa na burudani kutoka katika bendi ya Tanzanite. Alisema mbunifu mwingine wa Mavazi Farouque Abdella wa zanzibar atafungua pazia la maonesho hayo akifuatiwa na mbunifu Mago ambapo wadhamini mbalimbali wakiwemo PSI Tanzania, 361 degree Events na Mstapha Hassanali Couture wamejitokeza kudhamini maonesho hayo. "Wagonjwa wana kila sababu ya kujifunza na kuishi katika mazingira ya kupendeza lakini tunahitaji msaada na mimi kwa kushirikiana na wenzangu tutashiriki kikamilifu katika onesho hilo kuchangisha fedha," alisema hassanali.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers