Chama
cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi ya kupatiwa Hati
ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja ili
aweze kucheza mpira wa miguu nchini humo.
DFB
imetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili
kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer
FuBall-Verband ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani
nchini humo.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Mashindano wa DFB, Markus Stenger, Mtanzania huyo
ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi
kusajiliwa na klabu yoyote nchini.
TFF
inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya
taratibu husika kukamilika ikiwemo kubaini kama kweli mchezaji huyo
hakuwahi kusajili na klabu yoyote hapa nchini.
No comments:
Post a Comment