Timu
ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) sasa itaivaa
Misri kwenye raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za 10 za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika
mwakani nchini Morocco.
Awali
Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya kwanza dhidi ya Kenya, mechi ya
kwanza ikichezwa Septemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Hata hivyo,
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) jana lilituma taarifa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likielezea kujitoa kwenye
michuano hiyo.
Serengeti
Boys itaanzia nyumbani Oktoba 14 mwaka huu, wakati ya marudiano
itachezwa nchini Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu. Mshindi baada ya
mechi hizo mbili ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla ya
kwenda Morocco.
Katika
raundi ya tatu ambayo mechi zake zitachezwa katikati ya Novemba na ya
marudiano mwisho mwa mwezi huo, mshindi kati ya Tanzania/Misri atacheza
na mshindi wa mechi ya Congo Brazzaville dhidi ya Msumbiji/Zimbabwe
ambazo zinapambana katika raundi ya kwanza
No comments:
Post a Comment