Hatimae katibu mkuu wa Shirikisho la soka
zanzibar(ZFA) asimamishwa kazi baada ya kungundilika kuwa hajui mambo mengi
yanayohusu elimu hasa kutokujua kutumia COMPUTER. Taarifa iliyotolewa na
mjumbe wa kamati tendaji ya ZFA Hafidhi ally Twahiri kwa niaba ya Rais
wa ZFA Aman Makungu ilisema sio kwa Katibu mkuu pekee ila yeyote atakae
kwenda kinyume na mabadiliko ya kutaka kuisafisha ZFA atasimamishwa
kazi. Taarifa hiyo imetolewa leo mbele ya waandishi wa habari katika
ukumbi wa zanzibar ocean view hotel.
No comments:
Post a Comment