Mshambuliaji wa liverpool, Luis Suarez, ana amini kuwa
analengwa sana na vyombo vya habari vya Uingereza lakini amekiri
alijiangusha katika mechi moja ya ligi kuu msimu huu.
Katika mahojiana na kituo kimoja cha habari cha
amerika ya kusini, mshambuliaji huyo kutoka Uruguay, amesema kila mara
yeye hufwatilwa pakubwa na mashirika hayo kwa kuwa jina lake huchangua
magazeti kuuza zaidi.
Suarez
ambaye ndiye mfungaji bora wa liverpool msimu huu huku akiwa amefunga
magoli 15, mawili nyuma ya nyota wa manchester United Robin van Persie,
amekiri alijiangusha wakati wa mechi yao na Stoke City tarehe saba
October mwaka uliopita.
Tangazo hilo la suarez limemuudhi kocha wa
liverpool brendan roggers, ambaye amesema, mchezaji huyo ataadhibiwa kuambatana na sheria za klabu hiyo.
Roggers, ametaja tangazo hilo la Suarez, kama moja ambalo kamwe halikubaliki.
Suarez sasa amewagadhabisha makocha wa timu zingine zinazoshiriki katika
ligi kuu ya Premier, na pia mashabiki ambao wanahisi kuwa mchezaji huyo
hujiangusha bila sababu.
Mwaka uliopita, mlinda lango wa Swansea, Ashley Williams, alisema
kuwa Suarez hujiangusha kuliko wachezaji wote ambao amewahi kucheza nao.
Mapema mwezi huu Suarez, alishutumiwa sana
kuhusiana na jinsi alivyofunga bao la pili la Liverpool, baada ya
kuunawa wazi mpira wakati wa mechi hiyo ya kuwania kombe la FA dhidi ya
Mansfeild Town.
Lakini kocha wa Liverpool, alimtetea mchezaji
huyo akisema kwamba aliunawa mpira bila kukusudia, lakini siku
iliyofuatia, vyombo vya hjabari vya Uingereza vilichapisha habari yenye
mada, Suarez ni mdanganyifu na mlaghai mkubwa.
Tangu alipojiunga na Liverpool mwaka wa 2011, mchezaji huyo ameandamwa na sakata nyingi.
Amepigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi
nane, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya
mchezaji wa Manchester United Patrice Evra na baada ya kumaliza adhabu
hiyo, alikataa kumsalimia Evra katika mechi iliyofuatia, hatua
iliyomkasirisha sana kocha wa Man United Sir Alex Ferguson.
No comments:
Post a Comment