Ulikua mwaka 1948, hospitali iliyo nje kidogo ya mji
mkuu wa London ilishuhudia mwanzo wa vuguvugu la mashindano ya walemavu,
baada ya daktari aliyekimbia utawala wa Nazi nchini Ujeremani mwenye
asili ya Kiyahudi kujaribu kubadili maisha ya wagonjwa walioathiriwa na
majeraha ya uti wa mgongo -- na hivyo kuwatia moyo washiriki michezo.
Michezo ya kwanza iliyojulikana kama "Stoke
Mandeville Games" ilipangwa mwaka 1948 ili ifanyike sambamba na
mashindano ya mwaka huo yaliyofanyika nchini Uingereza.
Jina
Mandeville ni la Hospitali ya huko Buckinghamshire ambako Prof. Ludwig
Guttmann aliongoza juhudi zake za tiba ya kiakili kwa wagonjwa wa uti wa
mgongo walioshiriki michezo ya mwaka huo, wakiwa wanaume 14 na wanawake
2 walioshiriki wakiwa ndani ya magari ya walemavu na kushiriki
mashindano ya kulenga mishale.
Wengi wao walikua ni wanajeshi waliojeruhiwa katika vita vikuu vya pili vya Dunia.
Mwaka mmoja baadaye timu sita zilishiriki
michezo huko Stoke Mandeville -- kukiwa na mashindano ya netiboli,
mchezo uliotangulia mchezo wa kikapu -- wakati michezo ikitumiwa kama
sehemu ya matibabu ya wagonjwa kama ilivyopengekezwa na Guttmann.
Mwaka 1956, ''taarifa ya dhamira''ilizinduliwa
kwa ajili ya Michezo hii ambayo wakati huu ilikuwa ni ya Kimataifa kwa
mujibu wa wavuti ya kumbukumbu za Mandeville inayodhaminiwa na mamlaka
ya wilaya hiyo
Taarifa hiyo ilisema 'dhamira ya michezo ya Stoke Mandeville ni
kuwaunganisha wanaume kwa wanawake waliopooza viungo kutoka sehemu zote
za Dunia katika vuguvugu hili la michezo ya Kimataifa, pamoja na moyo wa
wanamichezo hii leo kuwapa matumaini na kuwa kivutio kwa maelfu ya
walemavu.
Miaka minne baada ya hapo, wakivutiwa na
muongozo wa Guttman, mashindano ya kwanza ya Walemavu yakafanyika mjini
Roma sambamba na Olimpiki.
Miaka hamsini baada ya michezo ya kwanza kwa
walemavu, washiriki 4,280 kutoka mataifa 165 -- ikiwa ni idadi kubwa
kuwahi kujitokeza kushiriki -- wamerejea Uingereza kushiriki mashindano
ambayo hivi sasa yanashirikisha watu waliozaliwa na hali hio kutokana na
sababu mbalimbali labda ajali au kusababishwa na maradhi.
Tangu michezo hii ianzishwe huko Stoke
Mandeville, jina linalotumiwa na kibonzo mleta bahati mwenye jicho moja
au ''Mascot'' wa michezo, kwa hakika Michezo hii imepiga hatua kubwa.
Lengo la mashindano haya siyo kuwapima uwezo, bali kuwawezesha kufurahia uwezo wao moyo wa michezo hii umebaki pale pale.BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment