Nassoro Matuzya ni Mganga wa Tiba ya michezo kutoka INTERNATIONAL MEDICAL AND TECHNOLOGICAL UNIVERSITY cha Dar es salaam amesema kuwa viongozi wa vilabu lazima wawe na uelewa kuhusu maana ya kuwa na daktari husika wa timu na wawe wanamsikiliza pale anapotoa majibu kuhusu mchezaji kwani viongozi wamekuwa wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa kuwa na madaktari hasa kwa timu zao hivi karibuni shirikisho la soka la tanzania la kupitia katibu mkuu wa shirikisho Angetile Osiah kusimika rasmi zoezi la kuwapima wachezaji wanaotumia mihadarati ya kuongeza nguvu katika michezo hasa matumizi ya bangi kwa kisingizio kuwa bila bangi hawawezi kucheza, tff ilisema kuwa haitatoa taarifa kuhusu rasmi siku ambayo watakuwa wanapima watakuwa wakichukuliwa bila mpangilio maalum
SIKIZA HAPA
Aidha kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho la kandanda la Tanzania SAAD KAWEMBA amesema lazima waganga wa timu wawe na mikataba na katika fomu ya usajiri lazima kuwe na saini ya mganga mkuu wa timu na lazima awe amekaa katika benchi la ufundi ilikuweza kuthibitsha kama anafaa kuendelea au kutofaa kuendelea kwa mchezaji aliyepo kiwanjani .
SIKIZA HAPA
No comments:
Post a Comment