Magoli mawaili yaliyofungwa kila kipindi yaliipa Nigeria ushindi katika kuwania taji la kombe la dunia la wanawake chini ya miaka 20 dhidi ya Jamhuri ya watu wa Korea katika mechi ya kundi B katika jiji la Saitama na kuongoza Kundi hilo.
Ngozi Okobi Ndiye alikuwa wa kwanza kufunga goli ndani ya robo saa ya mchezo wakati Desire Oparanozie Aliongeza goli la pili katika kipindi cha pili Nigeria ambayo ilikuwa ikichagizwa na mashabiki wao waliosafiri ilitegemea wachezaji kama
Francisca Ordega katika uapnade wa kulia ambaye alifanya kazi kubwa kumfanya Okobi kufunga .
Okobi, Ordega na Oparanozie walikuwa wakionekana kuwa wachezaji hatari zaidi ambapo waliwaweka wakati mgumu vijana hao wa korea ambao ni washindi wa pili katika 2010 , Japokuwa Jamhuri ya Korea , walijitahidi vya kutosha huku wakipiga pasi fupi lakini walishindwa kabisa kuhimili mikiki ya Nigeria .
No comments:
Post a Comment