Makore Mashaga
Katibu Mkuu BFT |
Onesmo Ngowi Rais TPBC |
Shirikisho la Ngumi
Tanzania (BFT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC}
zimekubaliana kuunda Kamati ya watu kumi (lO) ili kufufua na kuundeleza
mchezo wa ngumi
Tanzania.
Kamati hiyo ambayo itajumuisha
wajumbe watano (5) kutoka BFT na watano (5) kutoka TPBC
itakuwa chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa TPBC, Godfrey Madaraka Nyerere
na itaiwa"Kamati
ya Nyerere ya
Kufufua
na Kuendeleza
Ngumi Nchini"
"Kamati ya Nyerere ya
Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini"
itafanya kazi ya kuandika hadidu rejea za rasimu ya makubaliano ya pande zote mbili
ili ziweze kutumika
kama mwongozo wa makubaliano hayo.
Ushirikiano kati ya BFT na TPBC utaratibiwa na Katibu Mkuu wa BFT
Makore Mashaga pamoja na Katibu Mkuu wa TPBC Nemes Kavishe.
Wawili hawa watakuwa ndio wakuu wa Sekretariet ya "Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini" ambacho ndicho chombo cha kusimamia na kuratibu makubaliano haya.
Wawili hawa watakuwa ndio wakuu wa Sekretariet ya "Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini" ambacho ndicho chombo cha kusimamia na kuratibu makubaliano haya.
Ushirikiano kati ya vyama
hivi viwili ambavyo kimoja kipo kwenye ngumi zaridhaa na kingine kipo kwenye ngumi
za kulipwa ni ushirikiano unaolenga kubadili mwelekeo wa mchezo wa ngumi Tanzania.Kwa muda mrefu sasa mchezo
wa ngumi umekuwa ukikumbwa na matatizo mbalimbali ambayo yamepelekea kutokuwepo
na maendeleo yanayotegemewa na wadau wa ngumi Tanzania.
Ushirikiano
wa vyombo vyote vinavyoratibu ngumi hapa Tanzania utakuwa ni msingi imara wa
kujenga ari ya maendeleo ya ngumi hapa Tanzania.
Tanzania
imekuwa ikivurunda kwenye mashindano ya kimataifa karibu kila mchezo hivyo
ushirikiano wa vyombo hivi viwili vya ngumi utakuwa ndio msingi imara wa
kuendeleza mchezo huo Tanzania .
No comments:
Post a Comment