HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 September 2012

Djokovic uso kwa uso na Murray




 


Katika mchezo wa Tennis ya Marekani yaani US Open, Bingwa mtetezi wa mashindano haya Novak Djokovic ameingia fainali ya mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo na kujiweka tayari kupambana na Muingereza Andy Murray, kwa kumtwanga David Ferrer wa Uhispania 2-6, 6-1, 6-4, 6-2 mda mfupi uliopita.
Katika fainali ya kesho Djokovic atalenga ushindi wake wa sita wa mashindano makubwa il hali Murray ambaye ameshindwa na raia huyo wa Sebia mara 8 atajitosa uwanjani akitaka kuwa Muingereza wa kwanza kushinda mashindano ya kima hicho.
Kwa upande wa akina dada Fainali itachezwa saa chache zijazo kutokana na hali ya hewa iliyovuruga ratiba ya mashindano. Mmarekani Serena Williams atakabiliana na Victoria Azarenka.
Serena Williams ambaye ni bingwa mara kumi na nne wa mashindano hayo alifuzu kwa fainali hizo baada ya kumshinda Sara Errani kutoka Italia kwa seti mbili za 6-1, 6-2.
Naye Victoria Azarenka, alijikatia tikiti ya fainali hizo kwa kumshinda bingwa wa mashindano hayo mwaka wa 2006 Maria Sharapova, kwa sti mbili kwa moja za 3-6, 6-2, 6-4.
Fainali ya mashindano hayo kwa upande wa wanaume itachezwa hapo kesho.
Katika mashindano ya wachezaji wawili wawili Sara Errani akishirikiana na Roberta Vinci kuunda timu ya Italia waliendelea na msimu mzuri kwa ushindi wa mashindano ya ngazi ya 'grand slam' ya Marekani ama US Open.
Errani na Vinci waliwashinda Andrea Hlavackova na Lucie Hradecka kutoka Czech 6-4 6-2 katika mashindano ya wanawake kuongezea ushindi wao wa mashindano ya Ufaransa mapema msimu huu. Pia walishiriki na kufika fainali ya Australia
BBCSWAHILI 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers