HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 September 2012

KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JUMAMOSI HII

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila walitwangana mpambano wao uliofanyika morogoro hata hivyo ulizua utata baada ya mpambano huo kugubikwa na alama za mshangao ambapo cheka aliibuka na ushindi wa point mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana na kutafutana kwa muda mrefu watapoza kiu yao kwa mpambano la jumamosi ya kesho.

Akizungumza Dar es Salaam , promota wa pambano hilo Oswald Mlay amesema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba
.
Amesema pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano huo utakaoamua nani zaidi

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na   kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers