Klabu
zote zilizowekewa pingamizi za wachezaji kwenye usajili na zile
zilizoweka pingamizi zinatakiwa kufika kwenye kikao cha Kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kitakachofanyika kesho (Septemba 4 mwaka huu).
Kikao hicho kitafanyika kwenye ofisi za TFF kuanzia saa 6 kamili mchana, na kitakuwa chini ya uenyekiti wa Alex Mgongolwa.
Klabu
ambazo zimewekewa/ kuweka pingamizi na zitakiwa kuwepo kwenye kikao
zilikiwa na nyaraka zote kuthibitisha madai yao ni Azam, African Lyon,
Flamingo, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Oljoro JKT, Polisi Mara, Rollingstone
Multipurpose Ateclass Foundation, Simba, Super Falcon, Toto Africans,
Villa Squad na Yanga.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma (KRFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika juzi (Septemba 1 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Kigoma.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya KRFA
chini ya uenyekiti wa Omari Saleh Mkwarulo ambaye amechaguliwa kwa
kipindi cha kwanza.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu mkoani Kigoma kwa kuzingatia katiba ya KRFA
pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya KRFA na Kamati ya Uchaguzi ya
TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Omari Saleh Mkwarulo
(Mwenyekiti), Issa Bukuku (Katibu), Ahmed Msafiri Mgoyi (Mjumbe wa
Mkutano Mkuu TFF) na Mohamed Nassoro (Mwakilishi wa Klabu TFF).
Nafasi
za Makamu Mwenyekiti na Katibu Msaidizi zitajazwa kwenye uchaguzi mdogo
utakaofanyika baadaye baada ya waliogombea ambao hawakuwa na wapinzani
kushindwa kupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.
No comments:
Post a Comment