Kocha wa mpira wa miguu
Mahmoud el Gohary amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi huko Jordan shirika la habari la MENA limethibitisha
El Gohary ambaye ni moja kati ya alama kubwa ya soka la misri alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo pale ma Pharaoh walipocheza fainali zao za mwisho za kombe la dunia mwaka 1990 ambapo aliiiongoza timu hiyo kutoa suluhu ya goli moja kwa moja dhidi ya mabingwa wa ulaya mwaka 1988 uholanzi huko italia huku akipta umaarufu kwa kuwa na ngome ngumu kiwanjani
, El Gohary ndie aliyeipatia Misri kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1998 kule ougodougo Bukinafaso .
El Gohary aliwahi kufundisha timu za taifa za Oman ,Jordan na Misri ,na aliwahi kuifikisha Jordan hatua ya robo fanali katika kombe la asia mwaka 2004 na aliwahi kuwa mshauri katika shirikisho la soka la Jordan mwaka 2009
katika ngazi ya klabu ameshinda vikombe vya nyumbani na vya kimataifa akiwa na timu za mji mmoja wa Cairo
Al Ahly na Zamalek,ikiwa pamoja ligi ya misri na ligi ya mabingwa barani afrika vile vile aliwahi kuchezea vilabu vikubwa vya nchi hiyo
Al Ahly katika miaka 1955 na 1961, lakini majeruhi yalimsabisha astaafu soka
El-Gouhari ameacha mke na watoto wa tatu .
No comments:
Post a Comment