HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

25 September 2012

LIGI KUU ZANZIBAR IMEENDELEA JANA



Mzunguko wa tatu wa ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar (ZGPL), unatarajia kumalizika hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Amaan kisiwani Unguja, kwa kuzikutanisha timu za Zimamoto na Chuoni.

Timu zote hazina matokeo mazuri katika michezo yao miwili ya awali waliyocheza na hivyo kuufanya mchezo wa leo kuwa na ushindani wa hali ya juu kwa timu hizo.

Kumalizika kwa mzunguko wa tatu kunaifanya ligi hiyo sasa ihamie kisiwani Pemba kwa timu za Unguja kwenda kisiwani Pemba kucheza na timu za huko na hii ni kutokana na idadi ya timu za Pemba kuwa kidogo kuliko timu za Unguja.

Ligi kuu ya Zanzibar inashirikisha timu 12 na kati hizo 4 zinatokea kisiwani Pemba na Timu 8 zinatokea kisiwani Unguja.

Timu zinazotokea kisiwani Pemba ni Duma, Jamhuri, Mabingwa watetezi, Super Falcon na Chipukizi.

Timu zinazotokea kisiwani Unguja ni Bandari, Malindi, Zimamoto, Chuoni, Mundu, Malindi, Mtende Rangers na KMKM.


Timu iliyopanda daraja msimu baada ya kumaliza kinara katika ligi daraja la kwanza msimu uliopita Mtende Rangers ya Unguja imeendelea kuifukuzia Chipukizi ya Pemba katika msimamo wa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar (ZGPL).

Hapo jana katika kiwanja cha Amaan, mjini Unguja Mtende Rangers iliichapa Mundu ya Unguja goli 2-0 na kufikisha point 9 sawa na Chipukizi baada kushuka uwanjani mara 3.

Mabao ya Mtende Rangers yalifungwa na Himid Mussa katika dakika ya 56 na bao la pili likifungwa na Diku Juma katika dakika ya 63.









No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers