■NAYE ADONDOSHWA KWENYE DAKIKA YA PILI RAUNDI YA KWANZA
Mtanzania Rajabu Jumanne Maoja karibu amdondoshe chini bondia Gottlieb Ndokosho wa Namibia katika dakika ya kwanza ya raundi ya kwanza ya mpambano wao kugombea ubingwa wa IBF Afrika katika uzito wa unyoya (Featherweight)
Mpambano huo uliovutia maelfu ya wananchi wa Namibia ulifanyika katika ukumbi wa SKW jijini Windhoek, nchini Namibia na kusimamiwa na Rais wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi jana tarehe 29siku ya jumamosi.
Mtanzania Rajabu Jumanne Maoja alipigana vizuri na kuiwakilisha Tanzania vyema baada ya kuingia nchini Namibia akiwa na ari kubwa na kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Maelfu ya mashabiki waliojazana katika ukumbi wa SKW walimshangilia Maoja kila aliporusha konde kumpiga Ndokosho wakisema kwamba Watanzania ni ndugu zao kwa hiyo mabondia hao wawili ni wao wote!
Katika mpambano huo ulioanza saa tatu za usiku baada ya mapambano manne ya utangulizi mabondia wote waliingia ulingoni na nyimbo zao walizozipenda na kuanza mpambano huo kwa uangalifu wakisomana. Maoja ndiye aliyeanza na mfululizo wa makonde mazito akimnyemesha Ndokosho na kumpeperusha katika dakika ya kwanza tu.
Katika dakika ya pili sekunde 48 Ndokosho alimvizia Maoja na konde kubwa la kwenye nyonga lililompeleka mtoto huyo wa Maoja chini. Baada ya kuhesabiwa mara nane na kushindwa kuamka ndipo refarii wa mpambano huo Timo Haikonda kutoka Namibia kumaliza mpambano.
Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Windhoek alimvika Ndokosho mkanda wa ubingwa baada ya Rais wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi, Onesmo Ngowi kumkabidhi mkanda mtendaji huyo wa jiji kuu la Namibia lililo safi kuliko majiji yote barani Afrika.
Kitendo cha wimbo wa taifa wa Tanzania kuimbwa neno kwa neno na maelfu ya Wanamibia katika mpambano huo kilivutia sana na wengi walipohojiwa baadaye kwanini wanaujua wimbo huo kwa maneno walisema kwamba Tanzania ni mkombozi wa Namibia kwa hiyo ni azma yao kuujua wimbo wa taifa wa mkombozi wao.

No comments:
Post a Comment