Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba
na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.
Washabiki
11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh.
14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
Mgawo
mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna
wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh.
3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi
ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical
support) sh. 2,000,000.
Umeme
sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh.
4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh.
4,867,754.49.
Nayo
mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana
(Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
imeingiza sh. 50,435,000.
112 WASHUHUDIA MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING
Watazamaji
112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati
ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu)
Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mapato
yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na
sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh.
29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
Kamati
ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.
No comments:
Post a Comment