Wakati
uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA ukiwa umepangwa kufanyika
October 14, tayari makundi katika wagombea yameanza kuonekana ikiwa jaribio la
kupanga safu ya uongozi wa soka katika mkoa huo kinara katika fitna.
Nafasi zinazo
tarajiwa kugombewa ni mwenyekiti ambayo kuna jumla ya wagombea watano
wamejitokeza kuwania nafasi hiyo. Wanao wania nafasi hiyo ni mwenyekiti
anatetea nafasi yake Amin Bakhresa, Evance Aveva, Salum Mkemi, Frank Mchaki na Juma
Jabri.
Kwa upande
wa nafasi ya makamu mwenyekiti inawaniwa na wagombea wawili ambao Salum Mwaking’inda
na Gungulwa Tambaza.
Nafasi ya
katibu wamejitokeza wagombea watatu, ambao ni Msanifu Kondo, Saidi Tuli na
Hamisi Ambali.
Wanao wania
nafasi ya ujumbe wamejitokeza wagombea wawili ambao ni Shafii Dauda na Muhsin
Balhboo, wakati ambapo wanaowania nafasi ya ujumbe wa vilabu ni Mohamed Bhinda
na Benny Kisaka.
Nusa nusa za
Rockersports zimebaini kuwa tayari kumeanza kujengwa safu mpya ya uongozi ya
DRFA hata kabla ya uchaguzi huo haujafika , kwani kumekuwepo na kampeni za
chini kwa chini zikiendelea katika zoezi hilo huku baadhi ya wagombea wakipigwa
vijembe vya waziwazi ya kuwa hawana nafasi ya kuongoza soka DRFA.
Safu iliyo
katika nafasi ni mwenyekiti Aveva na makamu wake ni Gungulwa Tambaza. Katibu msanifu
Kondo, mjumbe Muhsini na mjumbe wa vilabu Mohamed Bhinda.
Kwa mujibu
wa ratiba ya kuelekea katika tarehe ya uchaguzi huo, leo Septemba 16 ni siku kuweka mapingamizi na mwisho wa kamati ya uchaguzi kupokea
pingamizi ni Septemba 20 saa 10 alasiri.
Hakutakuwa
na ada katika kuweka pingamizi, bali pingamizi zizingatie matakwa ya ibara ya
11(2) ya kanuni za uchaguzi.
Ratiba hii
inaonesha Septemba 26 ni fursa ya kukata rufaa iwapo maamuzi yaliyotolewa na
kamati DRFA hayakurishishwa na mrufaa na hiyo itakwenda kwa kamati ya TFF.
Kampeni kwa
wagombea zitaanza rasmi Oktoba 4, hadi13 ambapo Oktoba 14 itakuwa uchaguzi.
Kama ilivyo
ada katika miaka ya hivi karibuni chaguzi nyingi katika vyama vya soka kumekuwa
na wagombea waandishi wa habari ambao wamekuwa wakishinda nafasi wanazo wania
mara hii pia waandishi wa habari watatu wamejitokeza akiwemo Benny Kisaka, Shafii
Dauda na Salum Mkemi.
No comments:
Post a Comment