Ligi kuu ya Tanzania Bara imeanza hii
katika viwanja saba tofauti hapa nchini , ambapo mabingwa watetezi wa
taji, Simba walikuwa katika uwanja wa taifa ikifungua pazia la ligi
dhidi ya Afrikan Lyon imechomolza na ushindi wa mabao 3-0.
Simba imepata mabao yake kupitia kwa
mshambuliaji hatari Emmanuel Okwi bao lililopatikan katika kipindi cha
kwanza kabla ya bao la pili kuwekwa wavuni na mlinzi wa kulia Nassoro
Cholo.
Bao la tatu lilipatikana katika kipindi
cha pili kupitia kwa njia ya penati baada ya walinzi wawili wa Lyon
kumkwatua Emmanuel Okwi katika eneo la hatari na bao hilo kuzamishwa
wavuni na mshambiliaji Daniel Akufor.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika
kocha wa Simba Milovan Circkovic amesema ameridhishwa na kiwango cha
timu yake huku akipongeza kikosi chake kwa kuanza ligi hiyo na matokeo
hayo.
Amesema anatarajia nidhamu ya kimchezo
iliyoonyeshwa na kikosi chake itaendelezwa katika mchezo unaofuata ambao
Simba itakuwa ikicheza dhidi ya JKT Ruvu mchezo ambao utapigwa katika
uwanja wa Taifa.
Matokeo mengine mabingwa wa kombe la
Kagame Yanga wamekwenda sare ya bila mabao 0-0 na Tanzania Prisons
mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine pale mkoani Mbeya.
Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akikokota mpira huku mchezaji wa
Jacob Massawe akimnyemelea wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi ambapo Simba ilishinda
bao 3-0 Dhidi ya African Lyon .
ROCKERSPORT UNDSTAND
No comments:
Post a Comment