Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
vyama vya mpira wa miguu mikoa ya Kilimanjaro (KRFA) na Manyara (MARFA)
katika uchaguzi uliofanyika juzi (Septemba 22 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA na ule wa MARFA walivyo na imani kubwa
kwao katika kusimamia mchezo huo katika mikoa hiyo.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa kamati za utendaji za MARFA na
KRFA zinazoongozwa na Elley Mbise na Goodluck Moshi, kwani viongozi hao
wapya wana changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha wanaendesha
shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba zao na vyombo vya mpira
wa miguu vilivyo juu yao.
Pia
tunatoa pongezi kwa kamati za uchaguzi za IRFA na MARFA na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa
kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa kuongoza MARFA ni Elley Mbise (Mwenyekiti), Wilson
Ihucha (Makamu Mwenyekiti), Apollinary Kayungi (Katibu), Peter Abong’o
(Mhazini), Khalid Mwinyi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Phortinatus
Kalewa (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Peter Yaghambe (Mjumbe).
Kwa
upande wa KRFA waliochanguliwa ni Goodluck Moshi (Mwenyekiti), Mohamed
Musa (Katibu), Kenneth Mwenda (Mwakilishi wa Klabu TFF), Kusiaga Kiyata
(Mhazini) na Denis Msemo (Mjumbe). Nafasi zilizowazi baada ya kukosa
wagombea wenye sifa kwenye vyama hivyo zitajazwa baadaye.
No comments:
Post a Comment