HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 September 2012

UTARATIBU WA KULEKEA MARACANA 2014 WAWEKWA WAZI LEO ZURICH


Shirikisho linalosimamia Mpira wa Miguu  Duniani kupitia kamati kuu, Alhamisi ya leo 27 september katika kikao kilicho fanyika Makao makuu ya Shirikisho hilo Huko Zurich Uswis  Kimepitisha Ratiba ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia 2014 Huko Brazil  ambapo mechi ya ufunguzi itachezwa Huko Sao paul june 12 na itaanza saa kumi na moja kwa saa za Brazil ambapo itakuwa saa saba za usiku kwa afrika mashariki 
 
Ambapo Mechi za makundi saa saba za Brazil ambazo ni sawa na saa tatu usiku kwa afrika mashariki na mechi ya mwisho kabisa itakuwa saa tatu usiku ambapo  kwa saa za afrika mashariki ni itakuwa saa kumi na moja alfajiri lakini afueni kwa watu wa afrika mashariki itaanza kuanzia hatua ya mtoano ambapo mechi zitakuwa zikichezwa kuanzia saa saba na saa kumi na moja za Brazil ambazo ni saa tatu usiku na saa saba usiku kwa saa za afrika mashariki wakati nusu fainali itachezwa kuanzia saa kumi na moja za Brazil ambap afrika mashariki itakuwa saa saba za usiku Mechi ya fainali itachezwa kwenye uwanja maarufu zaidi Nchini Brazil Maracana july 13 saa sita usiku kwa saa za afrika mashariki ambazo ni saa na saa kumi jioni kwa saa za Brazil

UWANJA WA MARACANA BRAZIL ITAKAPOCHEZWA MECHI YA  FAINALI YA KOMBE LA DUNIA 2014 

Aidha shirikisho hilo limeongeza kuwa Baadhi ya Mechi zitachezwa Kuzingatia muda wa nchi husika ili watu waweze kutazama na  kuzipa kila Nchi za  Bara husika   kuona timu zao  kwa upande Mwingine Tarehe ya Mwisho la kuwasilisha majina ya wachezaji itakuwa Tarehe 19 May 2014 huku Nchi zitakazo husika katika fainali ya klabu Bingwa Barani ulaya  zitapewa Muda wa Mwisho wa Kuwaslisha Majina ambayo ni  Tarehe 19-25 May 2014 ambao watapa juma moja la Mapumziko Upangwaji wa Makundi wa utafanywa December 6 ,2013 huko Costa do Sauipe katika kitongoji cha  Bahia.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers