HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 October 2012

Dk James Read wa chuo kikuu cha Birmingham Waamuzi hubagua


Aguero kutoka Argentina alilalamika hivi majuzi kwamba waamuzi huwaonea wachezaji wa kigeni katika ligi ya Premier

Utafiti uliofanywa kuhusiana na uamuzi wa marefa uwanjani katika mechi za ligi kuu ya Premier, unaonyesha kwamba waamuzi kwa jumla huenda wakawachulia hatua wachezaji wa kigeni kwa asilimia 15, kinyume na vile wanavyoweza kuwaadhibu wachezaji wa Uingereza.

Maelezo ya utafiti huu, yaliyochapishwa pia katika mtandao wa kijamii wa Tweeter, unaonyesha waamuzi ni wepesi wa kuwaadhibu wachezaji wachezaji walio wachache nchini Uingereza umefanywa na vyuo vikuu vya Birmingham, Cambridge na Oxford, na ulitumia takwimu zilizokusanya na OPTA Sportsdata, katika misimu ya ligi mwaka 2006-07 na 2007-08.

Utafiti huo ulikagua mechi 760 kwa jumla.

Utafiti ulikusanya ushahidi kutoka kwa hatua zote za mchezo (kwa mfano katika kuangalia migongeo na chenga), katika mechi zote, na vile vile maelezo kuwahusu wachezaji, kwa mfano nambari wanayocheza uwanjani, umri wao, urefu na ukubwa wa mchezo (kwa mfano, mechi kuu ya watani wa jadi mtaani).

Kwa kukusanya takwimu mbalimbali, watafiti waliepuka dhana kwamba kuonywa mara kwa mara wachezaji fulani kulimaanisha mchezo wao ni hatari.

Kinyume na hayo, watafiti wanaamini kwamba kwa njia moja, uchunguzi wao ulithibitisha kuna hali ya waamuzi kubagua pasipo kukusudia.

Hii ni hali ya jamii moja katika jamii kuwa na mawazo kwamba kundi fulani huwa na tabia za kutoridhisha.

Dk James Read wa chuo kikuu cha Birmingham anaeleza: "Matokeo ya utafiti yanaonyesha dhahiri kwamba waamuzi wamo katika hali ya kuandikisha makosa ya wachezaji wa kigeni moja kwa moja, kwa kuwa ni wa kutoka kwa jamii za waliowachache nchini Uingereza.

"Kwa upeo mkubwa tuliangalia masuala mengi kama anavyocheza mchezaji, umri na nafasi yake uwanjani, na katika kila mechi. Kwa hiyo tuna imani kwamba uamuzi unaoafikiwa na waamuzi sio kutokana na hali ya mchezo, lakini ni kwa kuangalia masuala mengine."

Mchezaji wa Manchester City, Sergio Aguero, kutoka Argentina, hivi majuzi alilalamika kwamba wachezaji wa kigeni huonea na waamuzi katika mechi za ligi kuu ya Premier, wakijilinganisha na wachezaji wenzao Waingereza.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers