Picha na Mahmoud Zubeiry |
Rais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba kwa
sasa shirikisho lake linawaachia wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom watumie busara
kumalizana na klabu ya Yanga, juu ya mgogoro wao kuhusu nembo ya ligi hiyo.
Akizungumza
katika Mkutano wake maalum na Waandishi
wa Habari leo makao makuu ya TFF, kuhusu masuala ya uchaguzi wa vyama mbalimbali
vya soka nchini, Tenga amesema kwamba kwa kuwa msimu uliopita Vodacom
walimalizana na Yanga bila kulishirikisha shirikisho lake, na mwaka huu
wanawaachia pia.
“Kitendo
kilichofanywa na Vodacom mwaka jana, kumalizana na Yanga bila kutushirikisha
kuhusu utata wa nembo, sisi tulijua kitaleta matatizo baadaye, na kweli sasa
yametokea, na ndiyo maana unaweza kuona, sekretarieti yetu inalipeleka taratibu
hili suala,”alisema Tenga.
Tenga alisema
Vodacom ingewaacha TFF msimu uliopita wakaihukumu Yanga kwa mujibu wa kanuni,
hata msimu huu ingekuwa rahisi kwao kuingilia, lakini kwa kuwa msimu uliopita
waliingilia na wakaibadilishia klabu hiyo nembo, basi na msimu huu pia
wanawaachia wamalizane wenyewe.
Mwaka jana Yanga
waligoma kuvaa jezi zenye nembo ya wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom kwa sababu
zina nembo nyekundu hadi kampuni hiyo ikawabadilishia na kuwapa jezi maalum
zenye nembo nyeusi.
Mwaka huu pia,
Yanga wamekataa kubandikiwa nembo za Vodacom kwenye jezi zao kwa sababu ya
rangi hiyo nyekundu na jana wamecheza mechi ya sita bila kuvaa nembo ya
mdhamini, wakisistiza wabadilishiwe.
Wakati huo huo,
kanuni za Ligi Kuu zinasema timu itakayogoma kuvaa nembo ya mdhamini itashushwa
Daraja, ingawa tishio hilo la kanuni sasa linapozwa na kauli ya Tenga
leo.
bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment