HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 October 2012

HAKUKUWA NA UBAGUZI DHIDI YA UINGEREZA


Chama cha soka cha Serbia, kimekanusha kwamba matukio ya ubaguzi wa rangi yalijitokeza katika mechi yake dhidi ya England, ya wachezaji chini ya umri wa miaka 21, iliyofanyika Jumanne, kufuzu kwa mashindano ya Euro mwaka 2013.
Maafisa wa chama cha Serbia pia walimlaumu mchezaji wa England, Danny Rose, kwa rabsha iliyotokea baada ya mechi, na kwa kuonyesha tabia mbovu na isiyofaa michezoni.
Awali, Rose, mwenye umri wa miaka 22, alikuwa ameitaka Serbia "kupigwa marufuku", kwa kuzua matukio ya ubaguzi wa rangi uwanjani dhidi yake wakati wa mechi.
Chama cha soka cha England kimesema inafaa shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, kuchukua hatua kali zaidi kwa yeyote yule atakayepatikana kuwa na hatia katika kuhusishwa na matukio ya ubaguzi wa rangi.
"Yaliyofanyika kamwe hayana kisingizio, na hayakubaliki kabisa. Leo tutawasilisha malalamiko yetu rasmi kwa shirikisho la UEFA.
Connor Wickham alifunga bao katika dakika ya 90, na vijana wa England chini ya meneja Stuart Pearce kuweza kufuzu kwa mashindano ya Euro mwaka 2013, huku rabsha ikianza pande zote mbili, na zikiwahusisha wachezaji na vile vile maafisa wa timu, na wote wakirushiana vitu mbalimbali uwanjani.
Waziri wa Uingereza David Cameron ni kati ya wale walioongezea sauti yao kwa kusema UEFA inafaa kuwawekea 'vikwazo vikali' wale wanaohusishwa na ubaguzi wa rangi, naye waziri wa michezo Hugh Robertson, amemwandikia rais wa shirikisho la UEFA, Michel Platini, akisema vitendo hivyo vilikuwa vya "uchochezi mno na ubaguzi".

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers