Timu ya taifa ya Poland imeshindwa kurejea ushindi wa kihistoria pale ilipotoa suluhu ya kufungana goli moja kwa moja siku moja baada ya mechi yao ya kufuzu fainali za kombe la dunia iliyobidi ichezwe jana kuhairishwa baada ya kiwanja kujaa maji lakini suluhu hiyo imekuwa kama ushindi kwa timu ya Poland
Wayne Rooney alijaribu kulizamisha jahazi la poland katika dakika ya 15 kabla ya mapumziko akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona iliyopigwa na Steven Gerrard na kufunga goli la thelathini akiwa na jezi ya uingereza lakini poland ilirejesha goli hilo katika dakika ya Sabini ,Shukrani kwa beki wa Torino Kamil Glik, ambaye naye alifunga goli kwa kwa mpira wa kona .
No comments:
Post a Comment