Mwendeshaji baiskeli Alex Dowsett wa timu ya Sky, amesema Lance Armstrong ataendelea kukumbukwa kama mwendeshaji baiskeli mahiri ulimwenguni, licha ya madai dhidi ya Mmarekani huyo ya kutumia dawa za kuongezea nguvu michezoni.
Shirika la kupambana na utumizi wa dawa za kuongezea nguvu nchini Marekani, lilimpokonya medali zote saba alizokuwa amepata Armstrong katika mashindano ya baiskeli ya Tour de France.
Mwendeshaji Dowsett, kutoka Uingereza, na mwenye umri wa miaka 24, alisema: "Yeye bado ni mahiri katika mchezo huu. Mtu ambaye alikuwa na saratani aliweza kurudi tena katika mchezo, na kupata ushindi wa Tour de France.
"Nadhani yaliyompata sio muhimu, na sidhani ni mambo ya kujali."
Dowsett alijiunga na timu ya Sky mwaka 2011, kutoka timu ya Marekani inayofahamika kama Trek-LiveStrong, na iliyoanzishwa na Armstrong kama timu ya waendeshaji baiskeli chini ya umri wa miaka 23, akiwa na lengo la kukuza vipaji vya waendeshaji chipukizi.
No comments:
Post a Comment