HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 October 2012

MGANDA AINGIA KUMKABILI MASHALI

Bingwa wa Uganda MEDY SEBYALA ameingia nchini kwa ajili ya pambano lao na Bingwa wa taifa wa Tanzania THOMAS MASHALI ,katika pambano la Ubingwa wa Africa mashariki na kati litakalo fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel siku ya jumapili 14/10/2012.

Akizungumzia pambano hilo katibu mkuu msaidizi bw said chaku ambae alikuwa pamoja na rais wa TPBO bw Yasin abdallah wakati wa mapokezi ya bondia huyo aliefatana na mwalimu wake tokea Uganda,ni kuwa wamefika salama na wapo katika hali nzuri ya ushindani na muda wote mganda huyo Med sebyala alionekana mwenye kujiamini na kujitapa kuwa amekuja kumuangamiza toto tukutu au simba asiyefugika-Thomas mashali na kuondoka na mkanda wa ubingwa kwao.

Pambano hilo la ubingwa wa afrika mashariki litasimamiwa na organization ya ngumi za kulipwa nchini-TPBO chini ya yasin Abdallah'ustadh' na mabondia hao watapima uzito na afya kiujumla saa tatu asubuhi siku ya jumamosi 13/10/2012 hapohapo friends corner hotel na zoezi zima la upimaji litasimamiwa na katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim Kamwe na dr Donald Madono pia kutakuwepo na mapambano zaidi ya sita ya utangulizi

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers