HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 October 2012

Noor Sabri AANGUSHWA NA MABEKI WA IRAQ


Timu ya soka ta taifa ya Iraq ambayo jumanne itakwaana na   Australia ,iliweza kuizuia Brazil ndani ya dakika ishirini tu za mwanzo katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja usiofungamana na timu yoyote hapo jana huko nchini Sweden  . ambapo vijana hao walimudu kucheza dakika ishirini tu bila kufungwa lakini Baadae Neymar alimtengenezea goli safi   Oscar  na kufunga goli la ufunguzi, na hapo ndipo mafuriko ya mabao yalipofuata na kutimia idadi ya magoli sita kwa bila   6-0 .

Neymar alimtengeneza oscar mpira malidadi kwa ustadi wa aina yake katika dakika ya ishirini na mbili na ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo   alifunga goli jingine katika dakika ya 75 na kumtengenzea  Lucas Moura dakika ya 80th , na badae oscar alifunga tena goli katika dakikaka ya  27th kwa mkwaju mkali  .

Kaka aliipatia Brazil bao la Tatu katika DK ya 48 akipiga shuti kali kutoka kwenye engo ngumu zaidi akiwa anakimbia  . na kufanya kuwa siku ya furaha zaidi kwa mchezaji huyo katika kikosi cha Brazil ambaye huchezea   Real Madrid , ambaye alionekana mwepesi kiwanjani kama alivyokuwa A.C. Milan siku za nyuma . Hulk  naye alifunga goli katika DK ya 56 ambapo golkipa  wa IRAQ  Noor Sabri alishindwa kudaka mpira katika dakika ya 56th.

Matokeo hayo yamemuumiza sana  Sabri, ambaye alijitahidi vya kutosha kuzuia michomo mingi na kama sio umahiri wake golini Brazil ingeshinda zaidi ya mabao   10- hadi 12

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers