HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 October 2012

SIMBA 4-1JKT OLJORO



Timu soka  ya Simba ya Dar es salaam leo imewazamisha wanajeshi wa JKT Oljoro kwa bao 4-1, kwenye  mchezo wa ligi kuu  uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Simba ilijipatia bao la kwanza kupitia kwa Amri Kiemba dk 16 aliyeachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa JKT OljoroBaada ya bao hilo JKT waliliandama lango la Simba na kujipatia bao la kusawazisha kupitia kwa Paulo Nonga dk 29 kwani mabeki wa Simba walikuwa wametoka hivyo ikawa rahisi kwa Nonga kumpiga chenga Juma Kaseja aliyekuja kuucheza.

Kabla ya kwenda mapumziko Kiemba tena aliwanyanyua mashabiki kwa kufunga bao lingine baada ya mpira wa krosi uliopigwa na Nassoro Masoud.
Timu zilikwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-1 Baada ya kurudi mapumziko timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini dk 83 Emanuel Okwi akifungia Simba bao la tatu baada ya kupokea krosi safi toka kwa Nassoro Masoud "Cholo"

Kwenye muda wa nyongeza Simba ilijipatia bao la penalti lililofungwa na Felix Sunzu baada ya mlinda mlango wa JKT Oljoro kumfanyia faulo mbaya wakati akienda kufunga bao na mwamuzi kumwonyesha kadi nyekundu. Mpaka dk tisini zinamalizika Simba wameshinda kwa bao 4-1 hata hivyo JKT itajutia mchezo huu kwani wachezaji wake wawili walionyeshwa kadi nyekundu kutokana na kucheza mchezo ambao siyo wa kiungwana. Kocha wa JKT Mbwana Makata amesema timu yake imefungwa na mabao yaliyofugwa hana shaka nayo kwani timu imecheza chini ya kiwango na ni mchezo wa kwanza timu yake kupoteza.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers