HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 November 2012

BILA KUJUA HADUI POULSEA KUTANGAZA KIKOSI KESHO

Shirikisho la soka nchini TFF limefanya marekebisho ya ratiba ya michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara kutokana na kuwepo kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao utachezwa katika tarehe ya kalenda ya shirikisho la soka duniani fifa Marekebisho hayo yametangzwa leo na katibu mkuu wa shirikisho hilo Angetile Osea katika makao makuu ya shirikisho hilo.
 Taifa Stars itakuwa na mchezo tarehe 14/11/2012 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam japokuwa bado haijathibitishwa itacheza na nchi gani lakini ni vema marekebisho ya ratiba yakafanyika wakati huu wanaendelea na mchakato wa kuthibitisha timu ambayo itakuja nchini kucheza mchezo huo.

Mechi  ambazo zita athirika na mabadiliko  ya ratiba ni pamoja na mchezo kati  ya Simba na Toto Afrika, JKT Oljoro dhidi ya Ruvu Shooting pamoja na mchezo kati  ya Tanzania Prisons dhidi ya JKT Ruvu mechi  ambazo hapo kabla ilikuwa zichezwe tarehe 11/11/2012 na sasa imerejeshwa nyuma kwa siku moja.

Mchezo wa Yanga na Coast Union uliopangwa kuchezwa tarehe 11/11/2012  utaendelea kuchezwa katika siku hiyo kama ilivyokuwa umepangwa toka awali.

 sababu kubwa ni kwamba kocha mkuu Kim Poulsen ambaye anatarajia kutaja kikosi hapo kesho ameomba kupata siku mbili za maandalizi  ya mchezo huo na kwamba wao kama TFF wamewasiliana na kamati ya ligi kuijulisha juu ya hilo na kimsingi imekubali kufanyike mabadiliko ya ratiba ili kutoa fursa kwa mtaalamu huyo kuandaa kikosi chake.

Osea " kuna umuhimu wa kucheza mchezo wa tarehe ya FIFA kuliko kutokucheza na kwamba usipocheza mchezo katika tarehe hiyo athari yake ni kupoteza alama za viwango vya ubora hivyo ni muhimu Tanzania ikacheza mchezo huo".

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers